ChatGPT Slides

Unda mawasilisho bora pamoja na timu yako na ChatGPT

Badilisha mazungumzo au kiolezo kuwa slaidi shirikishi. Alika timu yako ihariri na kutoa maoni, kisha uache ChatGPT au dot yako ifanye marekebisho. Wasilisha katika ChatGPT au hamisha kwenda PowerPoint au Google Slides.

Inapatikana kwa mipango ya Pro, Business na Enterprise.

Kihariri cha ChatGPT Slides chenye wasilisho kuhusu hali ya hewa, vijipicha vya slaidi, vishale vya washirika na kidirisha cha maoni ya pamoja.

Kuanzia taarifa za maendeleo ya timu hadi mawazo makubwa

Slaidi za kampeni bunifu zinazoonyesha miongozo ya chapa, mitindo ya maandishi, rangi zinazotumika na picha.

Mawasilisho bora bila kufanya kila kitu mwenyewe

Yape mawazo yako uhai

ChatGPT inaweza kukusaidia kubadilisha mawazo yako kuwa wasilisho bora kwa kuunda picha maalumu au kutumia picha unazopakia.

Tumia muda mfupi zaidi kufanya marekebisho

Fanyia kazi maoni pamoja na wanatimu wenzako katika wasilisho moja, na uombe ChatGPT isaidie kufanya marekebisho.

Anza na kiolezo chako mwenyewe

Shiriki mfano wa wasilisho na ChatGPT ili kuongoza mtindo na mpangilio wa slaidi zako.

Endelea kufanya kazi kwa zana unazopenda

Endelea katika kihariri cha mawasilisho unachopendelea, ukiwa na maudhui yanayoweza kuhaririwa na kuendelea kuboreshwa.

Unda wasilisho lako kwa hatua nne

Omba ChatGPT ibadilishe mazungumzo, faili au muhtasari kuwa slaidi, au anza kwa kutumia kiolezo.

Kisanduku cha mazungumzo cha Slaidi mpya kina chaguo za kuunda kuanzia mwanzo, kubadilisha ukurasa, kuhariri wasilisho lililopo na kuanza kwa kutumia kiolezo.

Jaribu agizo ili kuunda na kuboresha slaidi zako

Undeni pamoja wasilisho lako bora lijalo